Friday, August 9, 2013

SIHITAJI MUME,MUME WANGU NI KAZI",NISHA...



MREMBO anayekuja juu katika uaandaaji wa filamu Bongo Salma Jabu ‘Nisha’ ametoa mpya pale alipotangaza kuwa hana mahusiano na mwanaume yoyote na kuonyesha pete yake aliyodai ndio mumewe akiongea na mwandishi aliyetaka kujua kuhusu maisha yake ya mahusiano na kumtaka msanii atumie fursa hiyo kumtambulisha mpenzi huyo ambaye anaye na kusema hana mwanaume.

“Unaiona pete hii kwa wengine ni ishara ya pingu au ndoa na mimi pete hii inasimama kama alama ya mume wangu lakini mume wangu mimi ni kazi yangu ya filamu na si kingine naipenda sana kazi yangu na kuona au kuhisi pengine kama nikiwa na mume anaweza kunizuia nisifanye kazi ambayo ndio hobby yangu,”anadai Nisha.
Nisha ni mwigizaji ambaye amekuwa akifanya vizuri katika utayarishaji wa filamu za vichekesho huku mara nyingi akimshirikisha mchekesha mkongwe nchini King Majuto Komedi alizoandaa Nisha na kutikisa ni Pusi na Paku, Tikisa na filamu ya Macho yangu, pia siku za nyuma iliwahi kuripotiwa kuwa msanii huyo kuwa na mahusiano msanii wa hip hop Ney wa Mitego kitu anachokipinga Nisha.

WASTARA ATOA SIRI ZA SHIJA KUMTAKA ILA AKAZIDIWA KETE...

Mwanadada Wastara ametoa siri ambayo alikuwa hajawahi kuizungumza katika maisha yake ya uhusiano, kisa hicho kinachofurahisha kinahusu maisha yake na marehemu mume wake na sababu iliyomfanya afunge naye ndoa.

"Unajua Shija domo lake lilikuwa zege kumbe alikuwa ananitaka lakini akashindwa kuongea hadi mwenzake Sajuki (marehemu mumewe) alipotuma maombi na kusikilizwa, Baada ya Sajuki kukamilisha kila kitu na kuwa mke na mume ndiyo aliponitonya  kuhusu habari ya Shija kuwa wakati wananifuata kumbe alikuwa ananitaka ila marehemu Sajuki akawa mjanja." alisema Wastara
Shija mweneyewe anasema kuwa wakati huo alipokuwa anamtaka Wastara yeye alikuwa makini na kazi hasa utayarishaji wa filamu na suala la mapenzi lilikuwa la ziada.