Wednesday, July 31, 2013

WILLIAM MTITU ANUNUA VIFAA VYA KISASA VYA FILAMU DUBAI(PHOTOS).

Msanii huyo maarufu nchini aliandika "Baada ya kufanikiwa kununua camera mpya kabisa ambayo inaweza kushuti quality ya 4K hapa twa-test pamoja na mtaalam wa kampuni ya Sony anaitwa Mohamed kutoka ofisi kuu Dubai hapa tukishuti mitaa/establish mbalimbali katika jiji la dubai "

Tuesday, July 30, 2013

Citizen TV’s BAHA (of Machachari) lands HOLLYWOOD role

Citizen TV’s BAHA (of Machachari) lands HOLLYWOOD role
























Citizen TV’s actor Kamau Mbaya, the son to the late Beth Mbaya a.k.a. Wanade of the Mother in Law fame has landed a potential deal to act in a Hollywood made movie.
According to sources, the star who features in the famed Machachari drama, has been approached by an American producer to act in an upcoming movie which will be going down in December

Saturday, July 27, 2013

TAZAMA PICHA ZA MOVIE STAR KAJALA AKIWA SOUTH AFRICA

 
Juzi mwigizaji wa bongo movie Kajala aliondokoka nchini kuelekea Afrika ya kusini kwa ajili ya safari binasfi ambayo pamoja na mambo mengine alitembelea shue ya uigizaji ya AFDA (AFDA the South African School of Motion Picture Medium and Live Performance) iliyopo nchini humo.



TAZAMA PICHA JINSI FILAMU YA BAD LUCK TOKA RJ COMPANY ILIVYOKUWA IKIANDALIWA NA JINSI MASTAR MBALI MBALI WALIVYOTEMBELEA LOCATION

BAD LUCK COMING SOON

Ile Sinema iliomshirikisha miss Tanzania mwaka jana Salha Israel, Muda si mrefu itaingia mtaani kwa kishindo inayokwenda kwa jina la BAD LUCK Wadau mzigo huu si wa kuukosa kama kawaida ya RJ Company uwa hawabahatishi kwenye kazi.

Staff wa RJ COMPANY wakiwa kwenye pozi kabla kazi kuanza..


   Maandalizi yakianza hapa steve shoo akiweka vitu sawa kwa ajili ya kuupika mzigo wa BAD LUCK ambayo kwa sasa ushakamilika kwa kuingia sokoni.

Baba Haji na Johari on set hatari sana mzigo huu wadau..

Lisa pia alikuwepo maarufu kwa jina la Batuli naye yuko ndani ya mzigo wa BAD LUCK.

 Director Adam Kuambiana.

  filamu hii imeongozwa na adam kuambiana hivyo na ray nae ambae ndio bosi wa kazi hii alipita kuwaangalia vijana wake wakifanya kazi kipindi hicho.....

   Batuli bila kukosa ndani ya nyumba ni hatari sana..



 Miss akifanya mambo yake kwenye Bad Luck.

  Batuli na Johari wakiwa On Set..

  Kazi ni ngumu sana Location. Wakati mwingine kunakuwa na kazi ngumu sana maana sio kazi ndogo kabisa tuwatieni moyo   msiwavunje moyo mapambano bado yanaendelea..

Uwoya alipita location kuangalia jinsi RJ COMPANY wanavyofanya kazi.

 Vijana kazini....

Esha Buheti on Set...

AMANDA NA BWANA MISOSI MAPENZI KUSHINEI WAPIGANA KIBUTI..!!


HATIMAYE wale wapenzi waliong’aa hivi karibuni, mwigizaji Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’ na Mbongo Fleva, Joseph Rushahu ‘Bwana Misosi’ wanadaiwa kumwagana rasmi
 
Habari kutoka chanzo  ambacho ni mtu wa karibu wa wapenzi hao, zilieleza kuwa Amanda na Bwana Misosi walishamwagana kimyakimya ikiwa ni baada ya kushindwa kuelewana kitabia.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Amanda ili aelezee ukweli kuhusu habari hizo ambapo alikiri kuwa ni kweli wameshaachana na hii ni baada ya kushindwana kitabia.

“Mimi na (Bwana) Misosi tumeachana muda mrefu tangu mwezi wa pili  baada ya kushindwana na katika uhusiano wa kimapenzi, nimejifunza kuwa wanaume siyo watu wa kuwaamini asilimia mia moja kwani baadaye unaweza kujuta,” alisema Amanda.

Kwa upande wake Bwana Misosi hakuweza kujibu moja kwa moja swali aliloulizwa bali alianza kwa kujikanyagakanyaga
Kwanza niko safarini, je, ni nani aliyekuambia hizo habari….hebu ngoja nimpigie huyo Amanda nimuulize nani aliyetoa siri hiyo,” alisema Misosi

HIVI NDIVYO DUDE WA BONGO MOVIE ALIVYONASWA NA DEMU MWINGINE WAKILA RAHA

STAA wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amenaswa na demu mwingine aitwaye Mboni Mhando tofauti na mkewe anayeshi naye, Eva.
Dude na demu huyo aliyebainika kuwa ni msanii, walinaswa juzikati katika Hoteli ya Traventine Magomeni, jijini Dar wakijivinjari katika mikao ya kimalovee ambapo paparazi wetu alitumia kifaa maalum cha kupigia picha na kuwanasa bila wao kujijua.
Baada ya kuzinasa picha hizo, paparazi wetu alimvaa Dude na kumuuliza kulikoni agandane na demu huyo wakati ana mkewe nyumbani, alichomoa kuwa siyo demu wake bali ni msanii mwenzake eti wanapanga mipango ya kazi.

“Hapa tulikuwa tunapanga mipango ya kufanya filamu, huyu ni msanii tena wa siku nyingi sababu aliwahi kucheza kwenye Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu miaka ile,” alisema Dude huku akimsihi paparazi afute picha kama amekwisha piga.

Friday, July 26, 2013

KITALE ALAANI KUHUSISHWA NA MALI ZA SHARO, SOMA HAPA ALICHOKISEMA


Msanii  wa  Commedy nchini na muimbaji wa bongo fleva  Kitale  rais wa mateja, amekanusha taarifa zinazomuhusiha na mali za Marehemu Sharo milionea.
  Katika  A/C yake ya BBM Kitale ameandika 
  "mama wa marehemu sharo Milionea ametoa malalamiko juu ya kutokabidhiwa baadhi ya mali za marehemu Sharo.
 
   Waandishi bila kumuelewa mama, wao moja kwa moja wananihusisha na mimi kuwa nahusika.  Hii ni kwa watanzania wote, Marehemu Sharo Milioneaaliacha gari aina ya Oper, naom,ba kuwaambia watanzania ile gari haipo chini yangu, ile Gari ipo chini ya Muddy Suma, ambaye ni mwenye gari aliyopata nayo ajali Sharo na mama yake   Sharo kulalamika kwenye vyombo vya habari ni sawa na ni haki yake kwa sababu mwenye Gari aliahidi kusamehe, ila aliomba aachiwe mpaka atakaponunua gari nyingine. Kinachoshangaza sasa ni mwaka unakwenda gari haijauzwa wala nini  kwa hiyo mama anahisi mimi na Mudfy suma letu moja.  Hapana mzazi wangu mimi nipo pamoja na wewe, na watanzania wote naomba muelewe gari sinayo mimi,. maana kila muandishi ananiandama mimi.  Kitu ambacho mimi na Sharo tulishea ni move tu. Gari anayo Mudy suma sababu  yeye  ndiyendiye aliwezesha na kuhusu sofa anazo Mudy Suma"
 Tutamtafuta Mudy Suma ili aweze kuthibitisha haya.

Wednesday, July 24, 2013

IRENE UWOYA AMUANDIKIA JOHARI UJUMBE MZITO


Katika pita pita zetu leo hii tuliweza kupata ujumbe mmoja mzito na wa kutia moyo toka kwa mwanadada Irene Uwoya aliomwandikia mkongwe wa bongo movies nchini kwa upande wa kinadada Blandina Chagula maarufu kama Johari wiki chache zilizopita.
Ujumbe huu wa Irene ni ujumbe wa kutia moyo na unaweza kuwa kama “Motivation message” kwa wadada wengi hapa mjini ili badala ya kukaa na kuwaza kupata mali au mafanikio kwa njia za mkato au zisizo halali basi wafanye kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi.
Tukinukuu ujumbe huo Irene kwa Johari aliandika….
“Wewe nimwanamke wapekee...mchapakaz sana...atawaongeee vp kaza moyo...one thng u hav to know if God say yes no body I mean no body can say no...so don gv r f*ck
Hii inawahusu wadada wote jamani. Nyie ni wanawake wapekee, wachapakazi, kazeni moyo. If God say yes, nobody can say no (Mungu akisema ndio hakuna awezaye kusema hapana)

WEMA SEPETU ANUNUA GARI JIPYA LA PINK

Wema Sepetu amenunua gari jipya la rangi ya pink kutokana na maneno ya meneja wake Martin Kadinda aliyoandika facebook na kuweka picha ya Wema akiwa na gari hilo "
 
samahani kwa ubora wa picha kuwa hafifu....... Ila huyu dada anapenda pink kupitiliza..... haya she gat new pink Car.... mkutane barabarani..." aliandika Martin. Licha ya gari hilo kutotajwa gharama yake wema ni kati ya mastar wa kike wanaomiliki magari meng kwa sasa yakiwemo pia ya gharama kubwa anayomiliki Movie star huyo

IRENE UWOYA NA LUCY KOMBA WASHIKANA UGONI


NYOTA wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krrish’ ametoa kali ya mwaka baada ya kudai kwamba amemshika ugoni msanii mwenzake, Lucy Komba mara baada ya kuziona picha za msanii huyo akiwa na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ wakiigiza filamu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutokea nchini Swaziland, Uwoya amepinga vikali utetezi unaosemwa kwamba Lucy na Kataut walikuwa wakishuti filamu na anaamini kuwa msanii huyo ameamua kumzunguka na kutaka kuibomoa ndoa yake.

“Lazima kuna kitu kinaendelea kwani katika dunia hii sijawahi kuona filamu inayochezwa na watu wawili tu mwanzo mpaka mwisho, ninachotaka kusema  ni kwamba Lucy ana mpango wa kuiharibu ndoa yangu,” alisema Uwoya kwa hasira.


Uwoya amehoji usiri wa filamu hiyo na kila alipokuwa akimpigia simu mumewe alikuwa akimjibu kwamba yuko Rwanda kumbe alikuwa Bongo akiigiza filamu na Lucy.
 

“Kwanza Lucy ashukuru niko mbali, laiti ningekuwa karibu angenieleza vizuri kwa sababu hata yeye angeweza kunipigia simu na kunifahamisha ushiriki wa mume wangu kwenye filamu hiyo kwa kuwa namba zangu anazo, ilikuwaje hakufanya hivyo?” alihoji.

Kuonesha kwamba amechukizwa na kitendo hicho, Uwoya alisema kwamba akitua Bongo atamtafuta Lucy ili aweze kumshughulikia vizuri na ikiwezekana amuoneshe hiyo filamu waliyoigiza watu wawili tu.

“Nitatua Bongo siku si nyingi na cha kwanza ni kumtafuta Lucy, anieleze vizuri kuhusu filamu hiyo waliyocheza na mume wangu,” alisema Uwoya.

Filamu hiyo ambayo imekuwa maumivu makubwa kwa Uwoya, imechezwa na Lucy na Ndikumana tu mwanzo hadi mwisho na imepewa jina la Kwa Nini Nisikuoe.

Tuesday, July 23, 2013

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA LUCY KOMBA KUHUSU NDIKUMANA, WAIGIZA PAMOJA FILAMU YA KWANINI NISIMUOE.

Lucy Komba na Hamad Ndikumana
Muigizaji maarufu Swahiliwood Lucy Komba amemsifia Hamad Ndikumana(Kataut) ambaye ameigiza nae katika filamu mpya ya "Kwanini Nisimuoe" kuwa ana kipaji cha uigizaji tofauti na alivyofikiria mwanzoni kuwa inaweza kuwa shida kidogo wakati alipomfuata kwa ajili ya utengenezaji wa filamu hiyo. Ndikumana ni msakata kambumbu maarufu akiwa mwenyeji wa Rwanda na alimuoa muigizaji maarufu nchini Irene Uwoya miaka michache iliyopita ingawa kwasasa wanadaiwa kutengana.

Akichonga na Swahiliworldplanet kutokea nchini Denmark alipo sasa Lucy Komba alisema "Ndiku ana kipaji kusema ukweli wakati namchukua kufanya nae kazi nilijua nitapata nae tabu sana lakini ni tofauti na nilivyofikiria ni mtu mmoja kichwa sana yaani msanii ni msanii tu alicheza mpaka mwenyewe nilifurahi kwa kifupi ana kipaji cha uigizaji, maelekezo kweli nilimpa na kumfundisha nilimfundisha lakini uchezaji wake ulikuwa juu zaidi"

Lucy Komba ameibua waigizaji wengi maarufu wanaotamba sasa wakiwemo Jackline Wolper, Mzee Chillo na Irene Uwoya hivyo usije kushangaa Ndiku akifanya kweli kwenye kiwanda cha filamu. Filamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni muda sio mrefu

MAJANGA MATUPU BONGO MUVI. WAKATI WAKIOMBOLEZA MSIBA WA MR BOMBA,MSANII MWINGINE AJIRUSHA GHORA YA 5 NA KUVUNJIKA KIUNO NA MIGUU YOTE,AHITAJIKA KWENDA INDIA HARAKA!

 Msanii chipukizi wa Bongo Muvi nchini Gado Balotel  akiwa mwenye huzuni baada ya kuvunjika kiuno na miguu yote.

  Hapa kama inavyoonekanamiguu ya  Gado Balotel  na bandeji baada ya kuvunjika yote mara baada ya kujirusha toka ghorofa ya 5
  Mshare unamuonesha  Gado Balotel  akiwa kwenye kava la moja ya filamu zake alizocheka kabla ya kukumbwa na balaa hilo.
 Msanii na Kiongozi wa kundi la Bongo Muvi nchini JB ambae ameombwa na wasanii kuchangisha harambee haraka ili kupata fedha za kumsadia msanii mwenzao huyo anaeishi kwa mateso makali.
  Msanii na mwanamasumbwi wa zamani Fike Wilson ambae amepongezwa na wadau baada ya kujitolea kumsaidia msanii huyo, ambapo kwa sasa anaishi nyumbani kwa Fike huku akiwa anabebwa kupelekwa chooni na kurudishwa pia.
  Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Saimon Mwakifwamba nae pia ameombwa kuungana kwa pamoja na wasanii wengine kumsaidia msanii mwenzao anaishi kwa mateso makubwa usiku na mchana.
Na Livingstone Mkoi

Msanii nyota toka kiwanda cha muvi za kibongo nchini Maulidi Mfaume maarufu kwa jina la Gado Balotel sasa amekumbwa na balaa la aina yake baada ya kuvunjika miguu yote miwili pamoja na nyonga kuteguka baada ya kudondoka toka ghorofa ya nne alipokuwa akiigiza filamu ya msanii mwingine aitwae Baga.

 

Baada Xdeejayz na kituo cha luninga cha DTV kupata taarifa hizo lilipiga hatua ndefu hadi mahala anapojiuguzia msanii huyo ambako ni nyumbani kwa msanii Wilson Fike maeneo ya Home Alone Vijana Kinondoni na kuonana uso kwa uso na msanii huyo aneishi kwenye maumivu makali.

 

Akiongea na mwandishi wetu nyumbani hapo Balotel alisema alikutwa na balaa hiyo wiki mbili zilizopita akiwa Location ndani ya hotel ya Con Way iliyopo Magomen Kagerana wasanii wenzake kama Hemed, Baga, Manaiki Sanga na wengineo wakati wakiigiza.

 

Balotel aliendelea kusema kuwa wakati shughuri za kuigiza ziliendelea na kuna sini moja iliyokuwa inahitajika kuigizwa kwa mfano ikimtaka mtu aigize kama anataka kujirusha kwenye ghorofa lakini asiruke ili kameraman  kuchukua picha achukue shoti hiyo kisha mtu huyo aende chini kisha achukuliwe shoti nyingine ya kujifanya ametua chini.

Msanii huyo aliendelea kusema kuwa nafasi hiyo ilibidi aigize msanii mwenye filamu Baga lakini kutokana na uwoga wa msanii huyo alikuwa akijishauri namna ya kuigiza kuruka ghorofani ndipo Ballotel akamtoa pembeni na kumuonesha namna ya kuruka kama Jet Lee huku akimwambie mwenzake hiyo ilikuwa kazi ndogo sana.

 

Msanii huyo aliendelea kusema kuwa baada ya hapo alijikuta ameruka toka ghorofa ya nne, lakini aliendelea kusema“ Wakati nikiwa bado sijashuka chini njiani nilianza kuhisi harufu ya kifo kwani tayari nimuona Israel mtoa roho akinipungia mkono na hatimae nilitua chini  kwa kufikia miguu” Alisema  Ballotel

 

Hata hivyo kijana huyo aliongeza kusema kuwa mala baada ya kutua nchini alihisi moto unawake miguuni mwake huku harufu ya damu ikimtoka puani na mdomoni na baada ya kujiangalia aliona visigino vyake vikiwa vimepasuka vyote huku tumboni kukiwa na maumivu makali sana kumbe wakati huo nyonga ilikuwa imeachia huku miguu yake ikiwa imesogea tumboni.

 

Gado alisema baada ya tukio hilo wasanii wenzake walimchukua na kukmimbiza Hospital ya Mwananyamala mbapo dakika chache baadae walimkimbiza Muhimbili kwa matibabu zaidi.Msanii huyo ambae ametamba sana kwenye filamu kama Going Bongo,Msitu wa Hifadhi,Tumbo Joto na Escap ambayo alikuwa akiigiza siku ya tukio lililomkuta.

Aidha msanii huyo aliendelea kusema kwa sasa anaishi kwenye mateso makali huku wasanii wenzake wakishindwa kumpa ushirikiana “Hapa nilipo nalelewa na Fike Wilsoni ndiye anaenibeba kwenda chooni na kunirudisha kwa kweli hali yangu sio nzuri nahitaji msaada wa wasanii wenzengu, Wako wanaokuja kunirushia chochote kama

 

Kalapina,Young Killer na madaktari wanasema huenda wakanishauri kwenda India ili wakazirekebishe nyonga zangu” Alisema Gado na kuongeza kuwa anawaomba wasanii wenzake wasamalia wema kumsaidia kwani hali yake ni mbaya na huenda kwa mujibu wa madakatari wake akahitajika kupelekwa India ili kukinusuru kiuno chake la sivyo hatozaa tena kwa vile nyonga vimeshafyatuka.

Sunday, July 21, 2013

RAY, RAMMY GALIS NA NAJMA WAJA NA FILAMU YA FANS DEATH.

Rammy Galis, Vicent Kigosi(Ray) na Najma ambaye ni mwanamuziki wa Bongofleva na aliyewahi kudaiwa kutoka kimapenzi na Mr.Blue wanakuja na filamu ya Fans Death. Filamu hiyo inayotarajiwa kuingia sokoni muda si mrefu, maudhui yake yanakuuliza ni nani mkali kati ya superstar na na mtoto wa mjini! Ray na Rammy Galis wakijaribu kumdaka Najma ikiwa msichana huyo ni ndugu wa damu na mmoja kati yao. Je ni nani huyo

SHILOLE ATANGAZA BIFU LA NGUMI BAADA YA SINTAH KUMPONDA KUWA ANAUWEZO MDOGO KIMUZIKI


MWIGIZAJI wa kike wa filamu na muziki Bongo zuwena Mohamed ‘Shilole’ amemtangazia hali ya hatari msanii mwenzake wa filamu na mtangazaji wa televisheni Christina John ‘ Sintah’ kuwa popote atakapomkuta lazima amchape kwa kipigo ambacho hatasahau katika maisha yake...

Shilole  ametoa kauli hiyo kufuatia kuandikwa na mwanadada huyo katika mtandao wake akimbeza kwa kejeli. .
“Ni kweli sisi wanawake hatupendani na kuwa na wivu wa kijinga, mtu anakurupuka anakotoka bila hata kufanya utafiti na kunibeza eti sina uwezo wa kuimba na JLO (Jenifer Lopez) ....

"Kuna mtu aliyetegemea mimi kwenda kufanya show Marekeni! Sasa ninachomwambia ninamtafuta nikikutana naye nimtapa kipigo cha Mbwa mwizi,”aliongea kwa hasira Shilole.

Katika mtandao wake Sintah aliandika kwa kusema Shilole ni sawa na mtu anayeota ndoto za mchana, na kumkejeli kwa kusema kuwa aendelee kuota anaweza baadae kurudi katika hali yake...

  Sehemu ya maneno yanayomkera Shilole ni haya: 
“Shilole bwana hii week katujia na kali kuliko eti ameongea na Benny Medina (Jlo’s Manager) ili aweze kufanya collabo na my sister, heee yes inawezekana maana hakuna lisilowezekana chini ya jua lakini swali ni?? wataimbaje?? yule dada yake na mie ni RnB na music wa Shilole bado sijaujua ni chakacha ama nini sasa naomba msaada kwenye tuta wadau wa music, hili linauwezekano??,”
 

“ Chakacha na RnB?? Kwa sababu Shilole nyimbo zake sawa na Snura wa majanga, kidogo Linah angeniambia ana collabo na my sisy ningeelewa sasa Shilole?? Ndoto za mchana ila si vibaya kuota maana ukishtuka unarudi ktk reality,”

Shilole anasema kuwa hajawahi kumuona mwanamke mwenye roho dhaifu kama Sintah, anajifanya anambabaikia Jlo wakati hata hajulikani....

“Mimi sikuwa nimeenda Marekani kwa ajili ya kuomba kumshirikisha J-lo kuimba naye,  lakini baada ya meneja wake kuja kuniona na kumpelekea video za muziki wangu  JLO alikubali kufanya kazi na mimi...

"Ilitakiwa nionane naye siku ya Jumapili lakini ndio siku niliyoondoka na ninarudi huko kwa ajili ya kazi hiyo, sijui nikifanya naye kazi atajificha wapi?,” anasema Shilole.

Shilole anasema Mungu ni mkubwa hata kama kuna mtu anayemchukia kwa mafanikio yake bado Mungu ana nafasi kubwa kuwazima watu wenye roho mbaya wivu kama Sintah ambaye anaonekana yupo tayari kwa ajili ya kuwaombea matatizo watu wanaojituma kwa ajili ya kuendesha maisha yao. 

Saturday, July 20, 2013

MSANII WA BONGO MOVIE ( MR. BOMBA ) AFARIKI DUNIA...MSIBA UPO BUGURUNI MALAPA- DAR


Msanii wa zamani wa Kundi la Kaole Sanaa. Mr Bomba amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na kansa ya uvimbe wa kwenye ini. 


Msiba utakuwa Buguruni Malapa jijini Dar es salaam nyumbani kwa marehemu alipokuwa akiishi. Mwili utaagwa siku ya Jumatatu nyumbani kwake Buguruni na kusafirishwa kijijini kwao Mpwapwa Dodoma siku hiyo ya Jumatatu kwa mazishi.

"WANAUME WALIO MSAIDIA SAJUKI WAMENIGEUKIA NA KUNITAKA KIMAPENZI"-WASTARA JUMA


Wastara Juma amefunguka kuwa wanaume wengi waliokuwa wakimsaidia wakati mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa mgonjwa wanamgeuka na sasa wanamtaka kimapenzi. 
 
Akizungumza kupitia Kipindi cha Take-One katika Runinga ya Clouds chini ya Zamaradi Mketema, Wastara alisema baadhi ya watu ambao walikuwa karibu naye wakati Sajuki anaumwa sasa hivi wamegeuka na kumtaka kimapenzi, jambo ambalo linamuumiza na kumshangaza mno.

Bishosti huyo alisema kuwa tofauti na wanaume hao ambao walikuwa wakimpa sapoti kipindi hicho, bado wapo wengine kibao kutoka nje na ndani ya nchi ambao wanatuma maombi kwake lakini anawaona wote ni matapeli na wanamtamani tu hivyo hayupo tayari kuingia kwenye uhusiano wa aina hiyo.

“Kweli ninaumia sana kwa sababu ninakaa na kujiuliza hawa wanaume walikuwa wanasubiri mume wangu afariki dunia ndiyo wanitongoze?
 

“Kusema kweli inanishangaza, hata watu ambao sikuwadhania kabisa eti nao wananitaka, watu wajue kwa sasa sipo tayari kuwa na mwanaume.
 

“Sitaki kukurupuka kwa sababu naweza nikaingia kwenye shimo la taka kwani jamii itanikimbia kutokana na kunuka, natamani kumpata mwanaume anayefanana na mume wangu kitabia.

“Uvumilivu wangu na uzuri ulitokana na kutunzwa siyo aje mtu anayetaka nikavumilie shida, hilo sitaki litokee, namuomba Mungu sana,” alisema.

Friday, July 19, 2013

MASHABIKI WAMPONDA WEMA SEPETU BAADA YA KUYAANIKA MATITI YAKE MTANDAONI

“Did I miss a spot…? I dunno,” ni maneno ya Wema kwenye picha aliyoiweka leo katika mtandao wa Instagram. 


Hata hivyo mashabiki wengi wamemshambulia mrembo huyo kwa kile wanachohisi hakupaswa kuiweka katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. 
 
Haya ni baadhi ya maoni:  

nanchesca5 Girl, I’m not trying to fix you,But this is the holy month.Keep it calm.It won’t hurt.

princesswawiey R u sure…ur a muslim? 1

khadijaumumustafa Wewe ni binti wa aina gani usieogopa mwezi mtukufu wa ramadhan ama kweli umeshindikana kabisa hata nachanguduwa uheshim huu mwezi ila wewe ni zaidi SubhanaLLAH.


sweettuma Punguza picha za hivyo vastaraa mwez ukiisha vaa utakavo jst jistir kwamda mfup hailet picha nzur .
 

mamu30 mhuu wema wangu ulivyokuwa na damu ya kunguni kesho tutaikuta hii picha kwenye mablog itakuwa gumzo ooh wema haheshimu mwezi mtukufu kumbe picha ya sikunyingi wao watadhani ndio unavyovaa hivi wakati wa mfungo lol
 

hazole Mnaolalamika mwezi mtukufu just unfollow her thn mwezi ukiisha rudini #GivePeopleSpaceToBreath

husnaomary Muislam mzma hata haushim mwez mtukuf wema….emu muogope Allah….picha gn hii na ramadhan hii….innallillah…nakupenda wema bt kumbuka kuwa huu mwez mtukuf…..heshma ishke mkondo wake…dis z Dunia baby…ickushikilie akili yako….nakupenda ndomana nakwambia.

hapnicole Mwenyezi Mungu anasema uwe msafi siku zote nd sio mwezi mmoja tu huo ni unafiki so bora yeye kuliko wewe unae mjaribu yeye kwa mwezi mmoja tu ni mtazamo

sele_yg Unanitega mwezi mtukufu..

noranuru what..ndo kuwatamanisha watu au ,mmh shoga namwezi huu wote..huchoki?