Saturday, July 27, 2013

TAZAMA PICHA ZA MOVIE STAR KAJALA AKIWA SOUTH AFRICA

 
Juzi mwigizaji wa bongo movie Kajala aliondokoka nchini kuelekea Afrika ya kusini kwa ajili ya safari binasfi ambayo pamoja na mambo mengine alitembelea shue ya uigizaji ya AFDA (AFDA the South African School of Motion Picture Medium and Live Performance) iliyopo nchini humo.



TAZAMA PICHA JINSI FILAMU YA BAD LUCK TOKA RJ COMPANY ILIVYOKUWA IKIANDALIWA NA JINSI MASTAR MBALI MBALI WALIVYOTEMBELEA LOCATION

BAD LUCK COMING SOON

Ile Sinema iliomshirikisha miss Tanzania mwaka jana Salha Israel, Muda si mrefu itaingia mtaani kwa kishindo inayokwenda kwa jina la BAD LUCK Wadau mzigo huu si wa kuukosa kama kawaida ya RJ Company uwa hawabahatishi kwenye kazi.

Staff wa RJ COMPANY wakiwa kwenye pozi kabla kazi kuanza..


   Maandalizi yakianza hapa steve shoo akiweka vitu sawa kwa ajili ya kuupika mzigo wa BAD LUCK ambayo kwa sasa ushakamilika kwa kuingia sokoni.

Baba Haji na Johari on set hatari sana mzigo huu wadau..

Lisa pia alikuwepo maarufu kwa jina la Batuli naye yuko ndani ya mzigo wa BAD LUCK.

 Director Adam Kuambiana.

  filamu hii imeongozwa na adam kuambiana hivyo na ray nae ambae ndio bosi wa kazi hii alipita kuwaangalia vijana wake wakifanya kazi kipindi hicho.....

   Batuli bila kukosa ndani ya nyumba ni hatari sana..



 Miss akifanya mambo yake kwenye Bad Luck.

  Batuli na Johari wakiwa On Set..

  Kazi ni ngumu sana Location. Wakati mwingine kunakuwa na kazi ngumu sana maana sio kazi ndogo kabisa tuwatieni moyo   msiwavunje moyo mapambano bado yanaendelea..

Uwoya alipita location kuangalia jinsi RJ COMPANY wanavyofanya kazi.

 Vijana kazini....

Esha Buheti on Set...

AMANDA NA BWANA MISOSI MAPENZI KUSHINEI WAPIGANA KIBUTI..!!


HATIMAYE wale wapenzi waliong’aa hivi karibuni, mwigizaji Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’ na Mbongo Fleva, Joseph Rushahu ‘Bwana Misosi’ wanadaiwa kumwagana rasmi
 
Habari kutoka chanzo  ambacho ni mtu wa karibu wa wapenzi hao, zilieleza kuwa Amanda na Bwana Misosi walishamwagana kimyakimya ikiwa ni baada ya kushindwa kuelewana kitabia.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Amanda ili aelezee ukweli kuhusu habari hizo ambapo alikiri kuwa ni kweli wameshaachana na hii ni baada ya kushindwana kitabia.

“Mimi na (Bwana) Misosi tumeachana muda mrefu tangu mwezi wa pili  baada ya kushindwana na katika uhusiano wa kimapenzi, nimejifunza kuwa wanaume siyo watu wa kuwaamini asilimia mia moja kwani baadaye unaweza kujuta,” alisema Amanda.

Kwa upande wake Bwana Misosi hakuweza kujibu moja kwa moja swali aliloulizwa bali alianza kwa kujikanyagakanyaga
Kwanza niko safarini, je, ni nani aliyekuambia hizo habari….hebu ngoja nimpigie huyo Amanda nimuulize nani aliyetoa siri hiyo,” alisema Misosi

HIVI NDIVYO DUDE WA BONGO MOVIE ALIVYONASWA NA DEMU MWINGINE WAKILA RAHA

STAA wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amenaswa na demu mwingine aitwaye Mboni Mhando tofauti na mkewe anayeshi naye, Eva.
Dude na demu huyo aliyebainika kuwa ni msanii, walinaswa juzikati katika Hoteli ya Traventine Magomeni, jijini Dar wakijivinjari katika mikao ya kimalovee ambapo paparazi wetu alitumia kifaa maalum cha kupigia picha na kuwanasa bila wao kujijua.
Baada ya kuzinasa picha hizo, paparazi wetu alimvaa Dude na kumuuliza kulikoni agandane na demu huyo wakati ana mkewe nyumbani, alichomoa kuwa siyo demu wake bali ni msanii mwenzake eti wanapanga mipango ya kazi.

“Hapa tulikuwa tunapanga mipango ya kufanya filamu, huyu ni msanii tena wa siku nyingi sababu aliwahi kucheza kwenye Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu miaka ile,” alisema Dude huku akimsihi paparazi afute picha kama amekwisha piga.