Baada ya kuzinasa picha hizo, paparazi wetu alimvaa Dude na kumuuliza kulikoni agandane na demu huyo wakati ana mkewe nyumbani, alichomoa kuwa siyo demu wake bali ni msanii mwenzake eti wanapanga mipango ya kazi.
Saturday, July 27, 2013
HIVI NDIVYO DUDE WA BONGO MOVIE ALIVYONASWA NA DEMU MWINGINE WAKILA RAHA
STAA wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amenaswa na demu
mwingine aitwaye Mboni Mhando tofauti na mkewe anayeshi naye, Eva.
Dude
na demu huyo aliyebainika kuwa ni msanii, walinaswa juzikati katika
Hoteli ya Traventine Magomeni, jijini Dar wakijivinjari katika mikao ya
kimalovee ambapo paparazi wetu alitumia kifaa maalum cha kupigia picha
na kuwanasa bila wao kujijua.
Baada ya kuzinasa picha hizo, paparazi wetu alimvaa Dude na kumuuliza kulikoni agandane na demu huyo wakati ana mkewe nyumbani, alichomoa kuwa siyo demu wake bali ni msanii mwenzake eti wanapanga mipango ya kazi.
“Hapa
tulikuwa tunapanga mipango ya kufanya filamu, huyu ni msanii tena wa
siku nyingi sababu aliwahi kucheza kwenye Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu
miaka ile,” alisema Dude huku akimsihi paparazi afute picha kama
amekwisha piga.
Baada ya kuzinasa picha hizo, paparazi wetu alimvaa Dude na kumuuliza kulikoni agandane na demu huyo wakati ana mkewe nyumbani, alichomoa kuwa siyo demu wake bali ni msanii mwenzake eti wanapanga mipango ya kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment