Wednesday, July 24, 2013

IRENE UWOYA AMUANDIKIA JOHARI UJUMBE MZITO


Katika pita pita zetu leo hii tuliweza kupata ujumbe mmoja mzito na wa kutia moyo toka kwa mwanadada Irene Uwoya aliomwandikia mkongwe wa bongo movies nchini kwa upande wa kinadada Blandina Chagula maarufu kama Johari wiki chache zilizopita.
Ujumbe huu wa Irene ni ujumbe wa kutia moyo na unaweza kuwa kama “Motivation message” kwa wadada wengi hapa mjini ili badala ya kukaa na kuwaza kupata mali au mafanikio kwa njia za mkato au zisizo halali basi wafanye kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi.
Tukinukuu ujumbe huo Irene kwa Johari aliandika….
“Wewe nimwanamke wapekee...mchapakaz sana...atawaongeee vp kaza moyo...one thng u hav to know if God say yes no body I mean no body can say no...so don gv r f*ck
Hii inawahusu wadada wote jamani. Nyie ni wanawake wapekee, wachapakazi, kazeni moyo. If God say yes, nobody can say no (Mungu akisema ndio hakuna awezaye kusema hapana)

WEMA SEPETU ANUNUA GARI JIPYA LA PINK

Wema Sepetu amenunua gari jipya la rangi ya pink kutokana na maneno ya meneja wake Martin Kadinda aliyoandika facebook na kuweka picha ya Wema akiwa na gari hilo "
 
samahani kwa ubora wa picha kuwa hafifu....... Ila huyu dada anapenda pink kupitiliza..... haya she gat new pink Car.... mkutane barabarani..." aliandika Martin. Licha ya gari hilo kutotajwa gharama yake wema ni kati ya mastar wa kike wanaomiliki magari meng kwa sasa yakiwemo pia ya gharama kubwa anayomiliki Movie star huyo

IRENE UWOYA NA LUCY KOMBA WASHIKANA UGONI


NYOTA wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krrish’ ametoa kali ya mwaka baada ya kudai kwamba amemshika ugoni msanii mwenzake, Lucy Komba mara baada ya kuziona picha za msanii huyo akiwa na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ wakiigiza filamu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutokea nchini Swaziland, Uwoya amepinga vikali utetezi unaosemwa kwamba Lucy na Kataut walikuwa wakishuti filamu na anaamini kuwa msanii huyo ameamua kumzunguka na kutaka kuibomoa ndoa yake.

“Lazima kuna kitu kinaendelea kwani katika dunia hii sijawahi kuona filamu inayochezwa na watu wawili tu mwanzo mpaka mwisho, ninachotaka kusema  ni kwamba Lucy ana mpango wa kuiharibu ndoa yangu,” alisema Uwoya kwa hasira.


Uwoya amehoji usiri wa filamu hiyo na kila alipokuwa akimpigia simu mumewe alikuwa akimjibu kwamba yuko Rwanda kumbe alikuwa Bongo akiigiza filamu na Lucy.
 

“Kwanza Lucy ashukuru niko mbali, laiti ningekuwa karibu angenieleza vizuri kwa sababu hata yeye angeweza kunipigia simu na kunifahamisha ushiriki wa mume wangu kwenye filamu hiyo kwa kuwa namba zangu anazo, ilikuwaje hakufanya hivyo?” alihoji.

Kuonesha kwamba amechukizwa na kitendo hicho, Uwoya alisema kwamba akitua Bongo atamtafuta Lucy ili aweze kumshughulikia vizuri na ikiwezekana amuoneshe hiyo filamu waliyoigiza watu wawili tu.

“Nitatua Bongo siku si nyingi na cha kwanza ni kumtafuta Lucy, anieleze vizuri kuhusu filamu hiyo waliyocheza na mume wangu,” alisema Uwoya.

Filamu hiyo ambayo imekuwa maumivu makubwa kwa Uwoya, imechezwa na Lucy na Ndikumana tu mwanzo hadi mwisho na imepewa jina la Kwa Nini Nisikuoe.