Msanii wa zamani wa Kundi la Kaole Sanaa. Mr Bomba amefariki dunia
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu
na kansa ya uvimbe wa kwenye ini.
Msiba utakuwa Buguruni Malapa jijini
Dar es salaam nyumbani kwa marehemu alipokuwa akiishi. Mwili utaagwa
siku ya Jumatatu nyumbani kwake Buguruni na kusafirishwa kijijini kwao
Mpwapwa Dodoma siku hiyo ya Jumatatu kwa mazishi.
Wastara Juma amefunguka kuwa wanaume
wengi waliokuwa wakimsaidia wakati mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa
mgonjwa wanamgeuka na sasa wanamtaka kimapenzi.
Akizungumza
kupitia Kipindi cha Take-One katika Runinga ya Clouds chini ya Zamaradi
Mketema, Wastara alisema baadhi ya watu ambao walikuwa karibu naye
wakati Sajuki anaumwa sasa hivi wamegeuka na kumtaka kimapenzi, jambo
ambalo linamuumiza na kumshangaza mno.
Bishosti huyo alisema kuwa
tofauti na wanaume hao ambao walikuwa wakimpa sapoti kipindi hicho, bado
wapo wengine kibao kutoka nje na ndani ya nchi ambao wanatuma maombi
kwake lakini anawaona wote ni matapeli na wanamtamani tu hivyo hayupo
tayari kuingia kwenye uhusiano wa aina hiyo.
“Kweli ninaumia sana kwa
sababu ninakaa na kujiuliza hawa wanaume walikuwa wanasubiri mume wangu
afariki dunia ndiyo wanitongoze?
“Kusema kweli inanishangaza, hata
watu ambao sikuwadhania kabisa eti nao wananitaka, watu wajue kwa sasa
sipo tayari kuwa na mwanaume.
“Sitaki kukurupuka kwa sababu naweza
nikaingia kwenye shimo la taka kwani jamii itanikimbia kutokana na
kunuka, natamani kumpata mwanaume anayefanana na mume wangu kitabia.
“Uvumilivu
wangu na uzuri ulitokana na kutunzwa siyo aje mtu anayetaka nikavumilie
shida, hilo sitaki litokee, namuomba Mungu sana,” alisema.