Friday, August 9, 2013

SIHITAJI MUME,MUME WANGU NI KAZI",NISHA...



MREMBO anayekuja juu katika uaandaaji wa filamu Bongo Salma Jabu ‘Nisha’ ametoa mpya pale alipotangaza kuwa hana mahusiano na mwanaume yoyote na kuonyesha pete yake aliyodai ndio mumewe akiongea na mwandishi aliyetaka kujua kuhusu maisha yake ya mahusiano na kumtaka msanii atumie fursa hiyo kumtambulisha mpenzi huyo ambaye anaye na kusema hana mwanaume.

“Unaiona pete hii kwa wengine ni ishara ya pingu au ndoa na mimi pete hii inasimama kama alama ya mume wangu lakini mume wangu mimi ni kazi yangu ya filamu na si kingine naipenda sana kazi yangu na kuona au kuhisi pengine kama nikiwa na mume anaweza kunizuia nisifanye kazi ambayo ndio hobby yangu,”anadai Nisha.
Nisha ni mwigizaji ambaye amekuwa akifanya vizuri katika utayarishaji wa filamu za vichekesho huku mara nyingi akimshirikisha mchekesha mkongwe nchini King Majuto Komedi alizoandaa Nisha na kutikisa ni Pusi na Paku, Tikisa na filamu ya Macho yangu, pia siku za nyuma iliwahi kuripotiwa kuwa msanii huyo kuwa na mahusiano msanii wa hip hop Ney wa Mitego kitu anachokipinga Nisha.

WASTARA ATOA SIRI ZA SHIJA KUMTAKA ILA AKAZIDIWA KETE...

Mwanadada Wastara ametoa siri ambayo alikuwa hajawahi kuizungumza katika maisha yake ya uhusiano, kisa hicho kinachofurahisha kinahusu maisha yake na marehemu mume wake na sababu iliyomfanya afunge naye ndoa.

"Unajua Shija domo lake lilikuwa zege kumbe alikuwa ananitaka lakini akashindwa kuongea hadi mwenzake Sajuki (marehemu mumewe) alipotuma maombi na kusikilizwa, Baada ya Sajuki kukamilisha kila kitu na kuwa mke na mume ndiyo aliponitonya  kuhusu habari ya Shija kuwa wakati wananifuata kumbe alikuwa ananitaka ila marehemu Sajuki akawa mjanja." alisema Wastara
Shija mweneyewe anasema kuwa wakati huo alipokuwa anamtaka Wastara yeye alikuwa makini na kazi hasa utayarishaji wa filamu na suala la mapenzi lilikuwa la ziada.

Thursday, August 1, 2013

CHUMBA ALICHOPELEKWA ROSE NDAUKA CHAKUTWA NA KONDOMU TANO ZILIZOTUMIKA


Chumba cha hoteli ambacho Rose Ndauka  alinaswa  akiingia  na  dogo  Nasry  ambaye  ni  msanii  wa  bongo  fleva, kimekutwa  na  kondomu  tano  zilizotumia...

Rose  Ndauka  ambaye  ni  mchumba  wa  Malik  Bandawe,wiki  iliyopita  alinaswa  akiingizwa  katika  chuba  hicho na  msanii Nassoro Ayoub  "Nasry".

Kwa  msaada  wa  wafanya  usafi  wa  hoteli  hiyo  iliyoko  maeneo  ya  kinondoni  jijini  Dar,wawili  hao  waliingia  katika  chumba  namba G17  cha  hoteli  hiyo  na  kutumia  masaa  takribani  matatu  huku  chumba  kikiwa  kimefungwa  na  walipotoka  chumba kilikuwa  hoi  bin  taaban....

"Mimi  ndiye  niliyefanya  usafi  chumba  namba  G17  siku  hiyo  na  nilikuta  kondomu tano  zilizotumika  huku  shuka  zikiwa  zimevurugika  kabisa."..Alifunguka  mfanya  usafi  huyo

Tukio  la  binti  huyu  kunaswa  akiingizwa  hotelini  na  dogo  Nasry  linatia  shaka  uchumba  wake  na  Malik Bandawe  ambaye  kwa  kipindi  kirefu  wamekuwa  wakitangaza  mipango  yao  ya  kufunga  ndoa

UWOYA NAKUJA KUWASHIKA, TV SHOW YANGU NI NOMA

uwoyair
Msanii bongomovie Irene Uwoya anakuja kwenye TV yako kwa njia nyingine tofauti na ya kiubunifu zaidi. Duniani kuna mastaa kadhaa ambao wanafanya reality show zao, lakini Irene Uwoya kupitia ukurasa wake wa Instagram ametoa news kwamba anaanzisha show yake binafsi kupitia kituo cha Clouds TV ambayo ni tofauti kabisa na show za mastaa wengine.
uwoya
  Undani kuhusu show hiyo ni kwamba kila kitu humo ndani kitahusu mambo ya nyumba. Irene na crew yake watakuwa na kazi ya kutembelea nyumba zenye hali mbaya na kuzifanyia ukarabati ili kuboresha hali ya mazingira ya kuishi ya muhusika mwenye nyumba au chumba. So, show yake itakuwa inaonyesha mwanzo nyumba ikiwa kwenye hali mbaya hadi atakapo ikamilisha na huo ukarabati. Hii picha inamuonyesha akiwa setting ku-shoot sehemu ya show hiyo.