WASTARA ATOA SIRI ZA SHIJA KUMTAKA ILA AKAZIDIWA KETE...
Mwanadada Wastara ametoa siri ambayo
alikuwa hajawahi kuizungumza katika maisha yake ya uhusiano, kisa hicho
kinachofurahisha kinahusu maisha yake na marehemu mume wake na sababu
iliyomfanya afunge naye ndoa.
"Unajua Shija domo lake lilikuwa zege
kumbe alikuwa ananitaka lakini akashindwa kuongea hadi mwenzake Sajuki
(marehemu mumewe) alipotuma maombi na kusikilizwa, Baada ya Sajuki
kukamilisha kila kitu na kuwa mke na mume ndiyo aliponitonya kuhusu
habari ya Shija kuwa wakati wananifuata kumbe alikuwa ananitaka ila
marehemu Sajuki akawa mjanja." alisema Wastara
Shija mweneyewe anasema kuwa wakati huo
alipokuwa anamtaka Wastara yeye alikuwa makini na kazi hasa
utayarishaji wa filamu na suala la mapenzi lilikuwa la ziada.
No comments:
Post a Comment